Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshugulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiw Ummy
Nderiananga amewasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kupokelewa na
Katibu Tawala wa Mkoa huo Missaille Albino Musa leo Novemba 4, 2024.
Mhe. Nderiananga licha ya
kusaini kitabu cha wageni amefanya mazungumzo na Katibu Tawala huyo kuhusu
masuala ya menejimenti ya maafa pamoja na uwajibikaji na utekelezaji wa
shughuli za Serikali mkoani humo.
Aidha, Mhe. Nderiananga yuko
mkoani Arusha kwa lengo la kuhudhuria Mkutano wa Afya Moja Tanzania unaofanyika
katika Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC) ukumbi wa Nyasa.
Mkutano huo unafanyika kuanzia
tarehe 04 hadi 06 Novemba, 2024.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.