Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema
msaada wa kifedha kwa ajili ya kusaidia walioathirika na kuporomoka kwa jengo
la ghorofa Kariakoo Jijini Dar es Salaam unatolewa kwa akaunti maalum ya maafa
ya 9921159801 ambayo ipo Benki Kuu ya Tanzania na kushughulikiwa na Ofisi ya
Waziri Mkuu.
Dkt. Yonazi ameyasema hayo leo
wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu hali inayoendelea katika zoezi
la uokoaji.
Amesema akaunti hiyo ni pekee
nchini ambayo inakusanya misaada ya kifedha kwa ajili ya maafa.
"Kuna watu wana nia njema
kabisa ya kuwasaidia Watanzania, lakini naomba tujizuie kabisa kukusanya
michango ya kifedha kutoka kwa mtu yeyote bila kupitia akaunti hii".
Amesema Dkt. Yonazi.
Aidha amesema akaunti hiyo ni
maalumu imethibitishwa na serikali ili kuweza kuhakikisha misaada inawafikia
walengwa na inatimiza malengo ya kutoa misaada hiyo.
Amesema kwa sasa operesheni
inaendelea mpaka pale watakapokamilisha zoezi la kuokoa baadhi ya watu ambao
bado hawajaokolewa.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.