WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka benki nchini zipunguze viwango vya riba
zinazotozwa kupitia mikopo mbalimbali wanayoitoa kwa wananchi.
Aliyasema
hayo jana jioni (Ijumaa, Februari 22, 2019) alipozungumza na wananchi
katika mkutano wa hadhara uliofanyika Bomang’ombe wilayani Hai.
Waziri
Mkuu ambaye yuko mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya kikazi alisema kitendo
cha benki kutoza riba kubwa kinawaumiza wajasiriamali nchini.
Pia,
Waziri Mkuu aliwataka wananchi hususani, vijana, wanawake na wenye
ulemavu kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa katika Halmashauri.
Alisema
kila halmashauri inatakiwa itenge asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili
ya kuwawezesha vijana, wanawake na wenye ulemavu kupata mitaji.
Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amewataka wakulima wa kahawa wabadilike na kuondoa miti ya zamani na kupanda mipya ili waongeze tija.
Waziri
Mkuu alisema wakulima hao wanaweza kuweka utaratibu wa kuondoa miche ya
zamani kwa awamu na kupanda mipya, hivyo kupata mavuno mengi.
(mwisho)
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.