WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Mkuu wa wilaya ya Biharamulo, Sada Malunde na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Wende Ng’ahara wamalize tofauti zao na wasipojirekebisha atamshauri Rais Dkt. John Magufuli kufanya maamuzi mengine.
Amesema
kitendo cha viongozi hao kutoelewana kinaonesha mfano mbaya kwa
watumishi walio chini yao, hivyo amewataka wajirekebishe mara moja kwani
wameaminiwa na Serikali kuliongoza eneo hilo na si kuwachanganya
wananchi.
Waziri
Mkuu ametoa kalipio hilo leo (Jumatano, Februari 20, 2019) wakati
akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja
wa mpira wa shule ya msingi Nyakanazi, kijiji cha Nyakanazi, Biharamuko
mkoani Kagera.
Amesema
kutokuelewana kwa viongozi hao ambao wakati mwingine wanatuhumiana
kufanyiana vitendo vya kishirikina kumesababisha kuzorota kwa shughuli
za maendeleo katika wilaya. “Mliletwa hapa kuiwakilisha Serikali na
kusimamia maendeleo ya wananchi nyie mnagombana.”
Awali,
Waziri Waziri Mkuu akiwa njiani kuelekea mkoani Kagera alitembelea
kambi ya Nyanza Roads inayojenga barabara ya Nyakanazi-Kabingo,
inayounganisha mikoa ya Kigoma na Kagera na kusema kuwa hajaridhishwa na
kasi ya mkandarasi huyo.
Barabara
hiyo inayojengwa kwa kiwango cha lami inaurefu wa kilomita 50 na
ilianza kujengwa 2014 ilitarajiwa kukamilika 2016, ambapo kwa sasa
ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 60.
“Sijaridhishwa
na kasi ya ujenzi wa barabara hii, mkandarasi na mhandisi mshauri wote
wanaonekana hawapo makini katika kufanya kazi hii. Hii ni aibu kwa
wakandarasi wa ndani ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia
kutokupewa kazi kumbe hawako makini.”
(mwisho)
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.