WAZIRI
MKUU Kassimu Majaliwa amesema hajaridhishwa na gawio la shilingi milioni 800
linatolewa na kiwanda cha Sukari cha Kilombero ambacho uzalishaji wake
ni kikubwa ikilinganishwa na kiwanda cha sukari cha Moshi TPC ambacho
kinatoa gawio la sh. billion 15 kwa mwaka.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Septemba 17, 2019) wakati
alipotembelea kiwanda hicho, akiwa katika siku ya nne ya ziara yake ya
kikazi Mkoani Morogoro. Amevitaka viwanda vya sukari nchini kuzaliza
sukari ya kutosha ili kukidhi mahitaji.
Akizungumzia
kuhusu vibali vya uagizaji wa sukari, Waziri Mkuu amesema Serikali
iliamua kutoa nafasi ya kuagiza sukari kwa wenye viwanda ili kuepuka
ujanja uliokuwa ukifanywa na baadhi ya wafanyabiashara ambao walikuwa
wakiagiza sukari kutoka nje ya nchi ambayo nyingine ilikuwa haina ubora.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amesema Tanzania bado kuna uhitaji mkubwa wa sukari
hususani ya viwandani, hivyo kusababisha Serikali kutoa vibali kwa
wamiliki wa viwanda kuagiza sukari kutoka nje ya nchi. “Viwanda vya
ndani vya sukari vihakikishe vinaongeza uzalishaji wa sukari ya
viwandani ili kukabiliana na upungufu uliopo.
Kwa upande wake, Naibu
Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba amesema mahitaji ya sukari kwa mwaka huu
nchini yameongezeka hadi kufikia tani 710,000 ikilinganishwa na tani
610,000 za mwaka jana.
Amesema
ongezeko hilo limechangiwa na kuongezeka kwa viwanda vipya vinavyotumia
sukari ya viwandani, ambapo kwa sasa mahitaji ya sukari ya viwandani
yamefikia tani 165,000.
Amesema
mahitaji ya sukari za majumbani kwa sasa ni tani 545,000, ambapo
kiwanda cha Kilombero kinazalisha tani 134,000, kiwanda cha Manyara tani
6,000, kiwanda cha Mtibwa tani 39,000 na TPC cha Moshi tani 100,000.
Naibu
Waziri huyo amesema ili kukabiliana na upungufu wa sukari Serikali
imeweka mkakati wa kuanzishwa kwa viwanda vipya vya sukari vya Bagamoro
ambacho kitaanza kuingiza awamu ya kwanza ya sukari sokoni tani 35,000
ifikapo mwaka 2022 na kiwanda cha Mkulazi kinatarajiwa kuzalisha tani
200,000 na cha Mbigili tani 50,000.
Akitoa
taarifa za kiwanda hicho Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari Balozi Amry
amesema Kampuni ya Sukari ya Kilombero imezingatia kikamilifu wito wa
Serikali wa kukuza uzalishaji na kuweka mipango thabiti ya upanuzi wa
uzalishaji wa kilimo cha miwa na kiwanda cha kusindika miwa. Mradi huo
utagharimu sh. bilioni 700.
Katika hatua nyingine,Waziri
Mkuu ametoa muda wa wiki mbili kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya
ya Kilosa awe amechimba visima katika kata ya Ruaha kwa ajili ya
kuwawezesha wakazi wa eneo hilo kupata maji safi na salama.
Ameyasema
hayo baada ya wakazi wa kata hiyo kusimamisha msafara alipokuwa
akielekea kata ya Malolo. Amesema halmashauri hiyo inakusanya zaidi ya
sh. bilioni mbili kwa mwaka hivyo inatakiwa kutenga kiasi cha fedha za
mapato kugharamia miradi ya maendeleo ya wananchi.
Waziri Mkuu amesemaSerikali inatekeleza Kampeni
ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani, ambayo
inalenga kuwaondolea wananchi tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji
safi na salama kwa kuhakikisha huduma hiyo inapatikana karibu na maeneo
yao.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.