Kamati ya Makatibu Wakuu
inayoongozwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),
Dkt. Jim Yonazi, imekagua na kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa uwanja mpya
wa kisasa wa mpira wa miguu katika eneo la Olmoti, jijini Arusha. Uwanja huo
unatarajiwa kuwa miongoni mwa viwanja vitakavyotumika kwenye mashindano ya
AFCON 2027.
Dkt. Yonazi amesema maendeleo
ya mradi huo ni ya kuridhisha na uwanja huo utakuwa si tu kituo cha michezo,
bali pia kivutio cha utalii na maendeleo ya uchumi kwa wakazi wa Arusha.
“Tunaamini uwanja huu utakuwa
fursa kwa wananchi kuwekeza kibiashara. Ujenzi huu unapaswa kutazamwa kama
chachu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi,” amesema Dkt. Yonazi.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu
wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, ametoa
shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan, kwa uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya michezo.
Naye Rais wa TFF, Wallace
Karia, amesema uwanja huo utaongeza idadi ya matukio ya kimataifa nchini,
Kutakuza vipaji vya ndani, na kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia michezo.
Ujenzi wa uwanja huo ni sehemu
ya maandalizi ya Tanzania kuandaa mashindano ya AFCON 2027, kwa ushirikiano na
Kenya na Uganda
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.