Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chombo kinachosimamia
utekelezaji wa Programu zinazofadhiliwa na Mfuko wa Dunia (Tanzania National
Coordinating Mechanism - TNCM) Dkt. Jim Yonazi ameongoza kikao cha wajumbe wa
chombo hicho kwa ajili ya kupitisha Maboresho ya Bajeti ya Utekelezaji wa
Programu za Malaria, Kifua Kikuu, UKIMWI ambayo ni mzunguko wa saba (GC7) kwa
mwaka 2024 hadi 2026.
Kikao hicho kimefanyika tarehe
10 Julai, 2025 katika Jengo la Tume ya Ushindani Jijini Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na wajumbe kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu,
Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI, Wizara ya
Fedha, Wizara ya Afya, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Medical Stores
Department (MSD), Local Fund Agent (LFA), Sekretarieti ya TNCM, Asasi za Kiraia
(Non State Actors - NSAs), Mashirika ya Kimataifa (WHO, UNAIDS), Wadau wa
Maendeleo (US Government, British High Commission pamoja na wawakilishi kutoka
Mfuko wa Dunia).
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.