Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi amefanya ukaguzi wa
maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yanayotarajiwa kufanyika tarehe
25 Julai 2025 katika Uwanja wa Mashujaa, Mtumba – Dodoma.
Maadhimisho hayo yatapambwa na
gwaride kutoka majeshi matano ya ulinzi na usalama na mgeni rasmi atakuwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika ziara hiyo, Waziri
Lukuvi aliambatana na viongozi waandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na
maafisa kutoka JWTZ na Jeshi la Polisi.
Maandalizi yameelezwa
kuendelea vizuri, huku tukio hilo likitarajiwa kuwa la kitaifa na kihistoria
katika kutoa heshima kwa mashujaa wa Tanzania.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.