Mke wa aliyekuwa Rais wa
Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, Mama Janeth Magufuli ametembelea
banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya
Kimataifa (SABASABA) Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na viongozi wa ofisi
hiyo.
Akiwa katika banda hilo, Mama
Janeth alipokelewa na kutembelea kuona namna Ofisi ya Waziri Mkuu inavyohudumia
wananchi kupitia Idara, Vitengo pamoja na Taasisi zake.
Aidha, miongoni mwa huduma
zinazotolewa na ofisi hiyo ni pamoja na elimu ya masuala ya menejimenti ya
maafa, shughuli za Wakala wa Kupigachapa Mkuu wa Serikali, Baraza la Taifa la
Biashara, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, elimu ya masuala ya
Vyama vya Siasa Nchini, Masuala ya VVU na UKIMWI, Usalama na Afya Mahala Pa
Kazi, Masuala ya Watu Wenye Ulemavu, programu ya ASDP II, fursa za vijana
pamoja na huduma zinazotolewa na NSSF, PSSSF, WCF na CMA.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.