Mkurugenzi wa Uratibu wa
Shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Paul Sangawe ameongoza
Kikao cha Kamati ya Wataalamu kuhusu matokeo ya tathmini ya kazi ya tafiti juu
ya kampuni zenye uwezo wa kujenga Meli kwa ajili ya Uvuvi katika Bahari Kuu.
Katika Kikao hicho, Bw.
Sangawe alilisitiza juu ya utekelezaji wa maelekezo ya Kikao cha Kamati ya
Usimamizi wa Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi kilichofanyika kabla ya
kikao cha wataalam. Masuala yaliyosisitizwa ni pamoja na upatikanaji kampuni
yenye uwezo wa kujenga Meli ya Uvuvi wa Bahari Kuu kwa viwango vinavyohitajika,
na kupata meli hizo kwa wakati ili kuchochea uvuvi wa kisasa nchini.
Vikao hivyo vya Programu ya
Kuendeleza Kilimo na Uvuvi ( AFDP) vimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Bluu, Zanziba
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.