WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.
Harrison Mwakyembe alifanyie mapitio Baraza la Michezo Tanzania (BMT)
na
iwapo hatoridhika na utendaji wake alivunje.
“Ninamuagiza
Waziri mwenye dhamana kufanya mapitio na kutathmnini upya utendaji kazi wa Baraza la Michezo Tanzania
juu
ya usimamizi wake wa michezo nchini na kama
hataridhika, anayo mamlaka ya kulivunja Baraza hilo.”
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Julai 5, 2017) katika hotuba yake ya
kuahirisha Mkutano wa Saba wa Bunge mjini Dodoma.
Amesema Serikali ya Awamu ya Tano
haitafumbia macho usimamizi mbovu na utawala wa michezo usiojali maslahi ya
Taifa. “Serikali imeazimia kuimarisha utendaji kwa vyombo
vya michezo nchini ili kila mwenye dhamana awajibike ipasavyo.”
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameipongeza timu ya vijana walio chini ya
umri wa miaka
17, Serengeti Boys iliyoshiriki na kutoa upinzani mkubwa kwenye mashindano ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Barani Afrika.
Amesema licha ya timu hiyo kumaliza
ikiwa na jumla ya pointi 4 sawa na timu iliyoshika nafasi ya pili, ila Vijana hao
wameonesha vipaji na uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yao.
“Msisitizo wangu kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni
kuendelea kuwatunza
vijana hao, na kusimamia vilabu vya michezo nchini kuwekeza kwenye soka la
vijana ili tujenge timu imara kwa miaka michache ijayo.”
Waziri Mkuu amesema Serikali
inatambua umuhimu wa michezo kwa afya, umoja wa kitaifa na kama fursa ya ajira
kwa vijana nchini.
“Wiki
iliyopita, mkoani
Mwanza yamehitimishwa mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA. Wananchi wa
Mwanza na Watanzania kwa ujumla wamejionea uwezo wa
kimichezo, vipaji na hamasa kubwa iliyopo miongoni mwa vijana wetu kutumia
vipaji vyao.
“
Amesema Serikali itaendelea kuratibu
michezo shuleni, ikiwa ni pamoja na kusimamia
ufundishaji wa michezo kama somo.
“Maelekezo yetu ni kwamba kila Mkoa uwe na shule angalau mbili zenye
mchepuo wa michezo na walimu wenye sifa stahiki za kufundisha michezo.”
Hata hivyo,
Waziri Mkuu amewaagiza
Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini, wahakikishe kwamba kila shule inakuwa
na viwanja vya michezo mbalimbali ili kuwapa fursa wanafunzi kushiriki michezo
ili kupandisha na kuinua vipaji vyao.
Pia Waziri
Mkuu alitumia fursa hiyo kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli kwa kuunga
mkono jitihada za michezo nchini kwa dhamira yake ya kujenga uwanja mkubwa wa
michezo mjini
Dodoma kwa kushawishi mataifa rafiki kama vile Morocco ambao wanajenga uwanja huo.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.