*Asema nchi ina utulivu wa kisiasa na uchumi
unaokuwa kwa kasi
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewahakikishia uwekezaji wenye tija wawekezaji
watakaokuja nchini kwa kuwa Tanzania ni nchi yenye amani, utulivu wa kisiasa na
uchumi wenye kukua kwa kasi.
Ameyasema
hayo leo (Jumapili, Julai 09, 2017) alipomuwakilisha
Rais Dkt. John Magufuli katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Aga Khan
alipochaguliwa kuwa Imamu Mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani.
Waziri
Mkuu amesema Serikali inatambua na kuthamini shughuli
mbalimbali zinazofanywa na mtandao wa taasisi za Aga Khan zilizopo hapa nchini,
hivyo Serikali itaendelea kushirikiana nao.
Ameupongeza mtandao wa taasisi za Aga Khan kwa kumuunga mkono
Rais Dkt. Magufuli katika kutoa kipaumbele cha kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji ili
waweze kujikwamua kiuchumi.
“Nawahakikishia
kwamba uwekezaji wenu hapa nchini utakuwa na baraka kwa sababu nchi imetulia kisiasa na uchumi
wake unakua kwa kasi. Nawaomba muendelee kuwaalika wanajumuia wa madhehebu ya Shia
Ismailia popote walipo duniani waje kuwekeza nchini fursa bado zipo.”
Kwa
upande wake Rais wa Jumuiya ya Madhehebu ya Shia
Ismailia Tanzania, Bw. Amin Lakhani ameishukuru Serikali kwa ushirikiano
inaowapa na kwamba ameahidi kuendelea kushirikiana nayo katika kuboresha sekta
mbalimbali nchini.
Amesema
mtandao wa maendeleo wa Aga Khan unatoa huduma mbalimbali zikiwemo za afya,
elimu, kilimo na kunaendesha miradi katika mabara ya Afrika na Asia kwa kuwapa
fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji ili kujikwamua
kiuchumi.
Awali, Mkuu wa wilaya ya Ilala, Bi. Sophia Mjema aliipongeza
taasisi hiyo kwa mpango wake wa upanuzi
wa hospitali na kuongeza vituo 35 vya afya kutoka 15 walivyonavyo.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.