WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi wa Shirika la Nyumba (NHC) kwa kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mnolela mkoani Lindi kwa muda mfupi.
Amesema ujenzi wa zahanati hiyo ya kisasa mwezi Machi,
2017 na sasa tayari kimekamilika, jambo ambalo litarahisisha upatikanaji
wa huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo na wa jirani.
Waziri Mkuu alitoa pongezi hizo
jana jioni (Alhamisi, Julai 13, 2017) alipozungumza na wananchi wa kijiji cha
Mnolela baada ya kuzindua zahanati hiyo iliyosimamiwa na NHC.
Alisema ujenzi wa zahanati hiyo ni muendelezo wa mkakati
wa Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha huduma za afya kwa kusogeza huduma karibu kwa wananchi wake.
“Rais wetu Dkt.
John Magufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi changamoto za mbalimbali
zikiwemo za huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono.”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa NHC, Bw. Nehemia Mchechu
alisema mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo ulisimamiwa na NHC na umegharimu sh.
milioni 65.5.
“Shilingi milioni 15 zilitolewa na Rais. Dkt. Magufuli,
sh. milioni 10 zilitolewa na Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye,
NHC ilitoa sh. milioni 10 na kiasi kilichosalia ni mchango wa halmashauri.”
Awali Mbunge wa jimbo la Mtama, Mheshimiwa Nape
alimshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa mchango mkubwa alioutoa katika mradi wa
ujenzi wa zahanati hiyo.
Mheshimiwa Nape alisema zahanati hiyo ni mkombozi kwa
wakati wa kijiji cha Mnolela na wananchi wengine wanaoishi kwenye maeneo yaliyo
jirani na kijiji hicho.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.