*Ni zile zilizotengwa kwa ajili ya maadhimisho ya Mashujaa
RAIS
Dkt. John Magufuli ameagiza sh. milioni 308 zilizotengwa kwa ajili ya
Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa, zitumike
kuboresha miundombinu ya barabara jijini Dodoma.
Ametaja
miundombinu hiyo ni pamoja na taa za kuongezea magari katika barabara
ya Kisasa na taa za barabarani kwenye barabara mpya ya Emmaus-African
Dream yenye urefu wa kilomita 1.4, ambayo kwa sasa inajengwa kwa kiwango
cha lami.
Taarifa
hiyo imetolewa na Waziri Mkuu leo (Ijumaa, Juni 29, 2018), wakati
akizindua kituo cha polisi kinachohamishika katika hafla iliyofanyika
eneo la Kisasa, jijini Dodoma. Kila ifikapo Julai 25 ya kila mwaka Tanzania huadhimisha sik u ya mashujaa.
“Sasa
kutokana na msongamano uliopo ambao unaweza kusababisha ajali,
Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Magufuli ameamua fedha zote
zilizoandaliwa kwa ajili ya maadhimisho hayo zitumike kuboresha
barabara,” amesema
Waziri
Mkuu amesema Rais Dkt Magufuli anawataka Watanzania wote waadhimishe
siku hiyo ya kumbukumbu ya mashujaa kwa kufanya usafi katika maeneo
yaliyo jirani na makazi yao pamoja na yale ambayo wamezikwa mashujaa
ikiwa ni njia ya kuwaenzi.
Kufuatia uamuzi huo, Waziri Mkuu amewaagiza Wakuu wa Mkoa waratibu zoezi hilo kwenye maeneo yao.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameliagizaJeshi la Polisi lianze kujikita kwenye matumizi ya mifumo ya kiulinzi ya kielektroniki yaaniCity Surveillance Sytemsili limudu kudhibiti hali ya sasa ya uhalifu.
Amesema kutokana na kuwepo
kwa mapinduzi makubwa ya kiteknolojia duniani, hususani kwenye nyanja
mbalimbali ikiwemo eneo la ulinzi wa raia na mali zao, hivyo ni wakati
muafaka sasa kwa Jeshi la Polisi lianze kutumia teknolojia za kisasa.
“Usimikaji
wa mifumo hiyo si tu utasaidia kupunguza uhalifu na kuongeza usalama wa
wananchi na mali zao lakini pia utaongeza imani kwa wafanyabiashara na
watalii wanaotembelea nchi yetu,” amesema.
Pia
Waziri Mkuu amewasisitiza wakazi wa eneo hilo kukitumia vizuri kituo
hicho ni kwa kupeleka taarifa za uhalifu. “Aidha, naomba niwasisitize
kituo hiki ni cha muda, hivyo uongozi wa eneo hili ni lazima uje na
mkakati wa kupata kituo cha kudumu,”.
Ufunguzi
wa kituo hicho ambacho ni kati ya vituo vitano vilivyogharimu sh.
milioni 250 vilivyotolewa na Benki ya Equity mkoani Dodoma; umehudhuriwa
na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.