NA
MWANDISHI WETU
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi (Idara ya Uhamiaji) imekusudia kufanya mabadiliko ya kimfumo
ambayo yatahusisha utoaji wa vibali ya ajira nchini pamoja na vibali vya ukaazi
ili kuhama kutoka mfumo wa zamani na kuwa na mfumo wa kielektroniki.
Maboresho hayo yanakwenda sambamba na
matumizi ya TEHAMA, ambapo kutakuwa na utaratibu wa kuwa na kadi moja (smart
card), ambayo itakuwa na taarifa za muhusika kuhusu kibali cha ajira pamoja na
hati ya ukaazi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama alikukutana na waandishi wa
habari hii leo Mjini Dodoma (Juni 28, 2018).
Waziri Mhagama alieleza
kuwa, kuanzishwa kwa mfumo huo utasaidia kurahisisha upatikanaji wa taarifa za
wageni nchini zenye uhakika na zitakazo patikana kwa wakati ili kudhibiti
mianya yote rushwa kwa watendaji kwa kuwa taarifa zote zitapatikana katika
kanzidata maalum.
“Uwepo na mfumo huu mpya
utasaidia kuondokana na mianya yote ya rushwa kwa Watendaji wa Serikali pamoja
na kurahisisha upatikanaji wa taarifa za wageni na malengo ya ujio wao hapa
nchini kwani taarifa zote zitapatikana kwenye kanzidata maalum,”alisisitiza
Mhagama
Kwa upande wake Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba alieleza kuwa mfumo huu wa kadi moja
utasaidia hutatua changamoto ya uchuleweshaji wa vibali ili kuondokana na
usumbufu wa ufuatiliji wa vibali hivyo kwa wageni.
“Lengo kubwa la mabadiliko
haya ni kuwa na kadi moja itakayomruhusu mgeni kufanya kazi kulingana na sheria
na taratibu zilizopo na kuwaondolea usumbufu usio wa lazima na kuongeza ufanisi
kwa watendaji wa Serikali,” alisisitiza Mwigulu
Aidha alitoa rai kwa Taasisi
zote zinazotumia wageni kuhakikisha wanafanya uhakiki wa taarifa za wageni hao
hususan uhalali wa kuwepo kwao pamoja na kazi wanazozifanya ili kuepuka udanganyifu
unaoweza kujitokeza.
“Nitoe rai kwa Taasisi zote
zinazotumia wageni katika ofisi zao kuhakiki na kujiridhisha taarifa za vibali
vya ajira na ukaazi wa wageni hao ili kuepuka taarifa zisizo sahihi na kuhakikisha
kila kila mgeni anakuwa na kibali halali kinachomruhusu kuwepo nchini,”alisisitiza
Mwiguli
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.