*Ataka apewe majina ya watakaokiuka agizo hilo
*Akataza magari ya Serikali kulala nyumbani kwa mtu
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya
Bahi mkoani Dodoma wanaoishi nje ya eneo lao la kazi wawe wamehamia
ifikapo Julai 30, mwaka huu.
“Tunataka
watumishi wa umma wawajibike na waishi katika vituo vyao vya kazi.
Nawataka watumishi wote wa wilaya hii wanaoishi Dodoma wawe wamehamia
hapa ifikapo Julai 30 mwaka huu na wasiohamia nipewe majina yao,”
amesisitiza.
Pia
ameagiza magari yote ya Serikali baada ya kuisha muda ya kazi yawe
yameegeshwa kwenye ofisi za halmashauri na ni marufuku kwa magari hayo
kulala nyumbani kwa mtu.
Ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Juni 27, 2018) wakati akizinduavituo
51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa, vituo 15 vya haidrolojia,
kanzidata ya taarifa za hali ya hewa na kituo cha operesheni na
mawasiliano ya dharura wilayani Bahi, Dodoma.
Waziri
Mkuu amesema Serikali inataka watumishi wote wa umma nchini waishi
kwenye vituo vyao vya kazi ili waweze kuwahudumia wananchi kwa ukaribu
katika maeneo husika.
Katika hatua nyingine,
Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bahi,
Bibi. Rachel Chuwa aanzishe mradi wa upimaji wa viwanja na viuzwe kwa
watumishi na wananchi kwa gharama nafuu.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.