Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi amewahamasisha na kuwahimza
viongozi wa Vyama vya Siasa juu ya umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi wa
Serikali za Mitaa.
Waziri amesema hayo wakati alipotembelea ya Makao
Makuu Vyama Vinne vya Siasa katika ziara yake iliyolenga kuendelea kuimarisha
mahusiano na falsafa ya Mhe. Rais. Dkt, Samia Suluhu Hassan ya 4R.
Amesema lengo ni kuvifikia
vyama vyote 19 kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa ikiwa ni pamoja na kutoa
salamu za upendo za Mhe, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwapa pongezi
viongozi wapya waliochaguliwa hivi karibuni.
“Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
unasimamiwa na TAMISEMI na una kanuni na taratibu za uendeshaji wake zinazohusisha Vyama vya
Siasa, hivyo natumia fursa hii kuhimiza wananchi wote kujitokeza kujiandikisha
katika zoezi linaloanza tarehe 11-20 /10/2024 kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali
za Mitaa ili wapate nafasi ya kuchagua na kuchaguliwa” alisema Waziri Lukuvi.
Aidha amewaomba viongozi wa
kisiasa kuendelea kutoa ushauri kwa Serikali bila kusubiri vikao vya baraza
vinavyoitishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa na badala yake wanaweza kupitia
Ofisi ya Waziri Mkuu kama kiungo ili waweze kuishauri Serikali wakati wowote.
Waziri Lukuvi amesema, “ni
wajibu wetu kudumisha amani na upendo kama alivyotuasa Mhe. Rais kwa kushindanisha
sera zetu kwa hoja na tukishapata matokeo tuwachie waliochaguliwa ambao watakuwa
ni Wenyeviti wa vijiji, Wenyeviti wa Mitaa na Wenyeviti wa Vitongoji watekeleze
wajibu wao.”
Nashukuru sana kwa sababu
vyama vyote wamekubali kutembelewa kwa ratiba ambayo itakuwa imepangwa,
Kwa upande wake Bi, Doroth
Temu Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT amesema wao kama wadau wanaendelea na
kazi ya msingi ya kuelimisha uma juu ya umuhimu wa uchaguzi na kuendelea kuwasilisha Serikalini maoni yote
wanayoyapata kwa wananchi.
“Tutaendelea kuwakumbumbusha
wananchi kwamba uchaguzi ni jukumu muhimu: na kuwahimiza kushiriki kwao kama raia wa Tanzania
katika kuchagua viongozi nasi tukitegemea uchaguzi kuwa huru na wakuaminika,”
alisema Makamu Mwenyekiti Bi, Doroth Temu.
Ikumbukwe kwamba katika siku
ya kwanza ya ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na
Uratibu) ametembelea na kukutana na Viongozi wa Vyama vya CHAUMMA, ACT
Wazalendo, CCK na UPDP.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.