Ameyasema hayo wakati
akifungua semina kuhusu ya masuala ya menejimenti ya maafa kwa Wahudumu wa Afya
Ngazi ya Jamii (CHW) katika Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza,
katika kuelekea Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa Dunia ambapo Kitaifa
mwaka huu yanaadhimishwa Mkoani Mwanza yakiwa na kauli mbiu isemayo “Elimu ni
Msingi katika Kulinda na Kuwawezesha Vijana kwa Mustakabali wa Baadae usio na
Maafa”.
Kwa upande wake Mratibu wa Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano kwa Maendeleo kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la ActionAid Bw.
Tema Hassan amesema masuala ya kukabiliana na maafa yanahitaji elimu mahususi
huku akisisitiza matumizi ya teknolojia ya kisasa ili kuifikia
jamii iliyokusudiwa.
“Teknolojia ni muhimu katika kuifikia jamii kiurahisi,
hivyo ni vyema kuwekeza katika matumizi ya simu na mifumo ya kisasa kwa
kuzingatia makundi yanayokusudiwa,” alisema Temu
Kufuatia hatua hiyo Bw.Temu amesema kuwa Shirika
la ActioAid litaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kukabiliana na
maafa nchini kwa kuzingatia unyeti wa masuala hayo na kuhakikisha jamii
inaendelea kuwa stahimilivu katika masuala ya maafa.
Kwa upande wake Afisa Afya wa Kata ya Kirumba Bi.
Veronica Massawe amesema usafi wa mazingira ni jambo lisiloepukika huku akiitaka
jamii kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu ili kujikinga
na magonjwa ya milipuko.
“Ni muhimu kulinda afya zetu kwani, Afya
ndiyo mtaji wetu sote" amesisitiza Bi. Veronica Massawe.
Ameongeza kuwa " Tumejiandaa, kukabiliana na maafa
ikiwa na pamoja na kujiepusha na mazingira hatarishi yanayoweza kutuletea maafa
katika kata yetu, usafi ni wajibu wa msingi kuwa na vyoo bora na kuvitumia
katika kupambana na magonjwa ya mlipuko"
Naye Mwenyekiti wa Wahudumu wa Afya ya Jamii Kata ya
Kirumba Bw. Wilfred Roman amesema watatumjia elimu waliyopewa katika semina
hiyo kwa kuwaelimisha wahudumu wa afya ngazi ya jamii kwa kufanya afya
shirikishi.
“Elimu tuliyopewa katika semina ni nyenzo muhimu
tutakayoitumia katika kupambana na magonjwa ya mlipuko,” amesema Wilfred.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.