Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe William Lukuvi ametoa rai kwa viongozi wa vyama
vya siasa viongozi wa dini viongozi wa kimila na viongozi wengine kushirikiana
katika kuhimiza wananchi kwenda kujiandikisha kwa sababu ni haki yao.
Wito huo umetolewa leo wakati
wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika katika Ukumbi
wa LAPF Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi wa vyama Siasa.
Ameeleza kwamba haki ya mtu
kujiandikisha inabaki pale pale awe mwanachama wa chama cha siasa au bila kuwa
mwanachama wa chama cha siasa.
Waziri Lukuvi amesema,
“tukijumlisha wanachama wetu wote kuna watu wanabaki ambao hawako kwenye fungu lolote katika vyama hivi vya siasa 19, lakini bado
tunao ushawishi wa kutumia sauti zetu kuhimiza
wananchi wote wenye umri wa kujiandikisha wajiandikishe na hatimae watumie nafasi hiyo kupiga kura”
Tunaowajibu kama viongozi wa
vyama vya siasa kwa pamoja kuufanya uchaguzi huu uwe mzuri.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Chama cha (UDP) Mhe. John Cheyo amesema kuna changamoto moja ya matumizi wa mhuri
wa chini ambao bado haieleweki vizuri, nadhani sisi kama wadau wa siasa tunayo nafasi
kukubaliana kwa kuwa na kauli moja ya kusimamia uchaguzi kulingana na kanuni na
sheria ambazo tumejiwekea.
“Tunadhamira ya kuwa na uchaguzi
huru na haki kwa kila mmoja wetu na kama ilivyoelezwa na Waziri Lukuvi na hiyo
ndiyo dhamira ya Mhe, Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassani,” alisema Mhe. Cheyo
Awali Makamu Mwenyekiti wa
Chama cha NCCR Mageuzi, Joseph Selasini amesema huu ni mkutano ambao
umeandaliwa tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili
kujipanga katika maandalizi ya chaguzi zinazoendelea.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.