Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi
ametembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia, ikiwa ni ziara yake ya
kikazi nchini humo, lengo ni kushiriki Kikao cha Tisa cha Jukwaa la Kanda la
Afrika la Kupunguza Athari za Maafa na Mkutano wa Nane wa Ngazi ya Viongozi
(High Level Meeting) kuhusu masuala ya kupunguza athari za maafa vinavyofanyika
Windhoek nchini Namibia.
Dkt. Yonazi ameambatana na
Timu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya
Maafa Ofisi hiyo Brig. Jenerali Hosea Ndagala, Mkurugenzi wa Tathmini na
Ufuatiliaji Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Charles Msangi, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa
ofisi hiyo, Bw. January Kitunsi pamoja na Afisa Habari wa Ofisi hiyo Bi.
Nyamagory Kitwara.
Aidha, katika mazungumzo na
mwenyeji wake ambaye ni Afisa Mambo ya Nje Mkuu na Kaimu Balozi wa Tanzania
nchini Namibia Bw. Elias Tamba ameeleza kuwa, nchi ya Tanzania itaendelea
kushirikiana na Naminia katika masuala mbalimbali kwa kuzingatia urafiki uliopo
baina ya Mataifa hayo mawili toka kipindi ya Uhuru wa Namibia ambapo Tanzania
inakumbukwa kwa mchango wake.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.