Thursday, April 8, 2021

Katibu Mkuu Nzunda ahimiza Kasi na Matokeo Ofisi ya Waziri Mkuu


 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) amewataka Manaibu Makatibu Wakuu wapya, Menejimenti  na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kuongeza kasi, bidii na ari katika utendaji kazi wa majukumu ili kutoa matokeo yenye tija  kwa wananchi.

Katibu Mkuu Nzunda ameyasema hayo leo tarehe 8 Aprili, 2021, Jijini Dodoma, wakati wa kuwapokea Manaibu Makatibu Wakuu wapya wa Ofisi ya Waziri Mkuu walioapishwa Ikulu Jijini Dar Es Salaam, Aprili 6, 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Ameeleza kuwa, Ofisi hiyo ina majukumu makubwa ikiwemo kuratibu shughuli za Serikali, hivyo ni muhimu kuongeza nguvu zaidi katika utekelezaji wa majukumu ili kusimamia kwa ufanisi uratibu wa shughuli za serikali.

“Jukumu letu ni kumsaidia Mhe. Waziri Mkuu kutekeleza majukumu ya kusimamia shughuli za serikali, hatunabudi kufanya kazi kwa utaalamu, weledi na kwa kuwajibika kwa kujituma ili kuhakikisha tunapata matokea anayo yataka,” alisema Nzunda

Kwa upande wa Manaibu Makatibu Wakuu wapya; Profesa Jamal Adam Katundu na Bw. Kaspar Kaspar Mmuya. wamemhakikisha Katibu Mkuu, kushirikiana na Watendaji wa Ofisi hiyo kwa  kufanya kazi kwa  kasi na weledi ili kuhakikisha changamoto za wananchi zinapata  ufumbuzi  kwa wakati.

Tarehe 6 Aprili, 2021 Ikulu Jijini Dar Es Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliwaaapisha Manaibu Makatibu Wakuu wa Ofisi hiyo.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya akipokea ua kutoka kwa Afisa Tawala wa ofisi hiyo Bi. Leah Kibasa wakati wa mapokezi alipowasili rasmi mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na watumishi wa ofisi hiyo Aprili 8, 2021 katika ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo Mtaa wa Relini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Jamal Katundu akipokea ua kutoka kwa Afisa Utumishi wa ofisi hiyo Bi. Faith Lazaro wakati wa mapokezi rasmi alipowasili na kupokelewa na watumishi wa ofisi hiyo Aprili8, 2021 katika ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo Mtaa wa Relini Dodoma.



Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar  Mmuya akisalimiana na watumishi wa Ofisi hiyo mara baada ya kuwasili rasmi katika ofisi hiyo, aliyeongozana naye ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa ofisi hiyo Bw. Greyson Mwaigombe.


Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu  Bw. Greyson Mwaigombe akimtambulisha Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Profesa Jamal Katundu kwa watumishi wa Ofisi hiyo eneo la Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu  mara baada ya kupokelewa katika ofisi hizo Mtumba Dodoma.



Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya akiweka saini kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda Jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Profesa Jamal Katundu akiweka saini katika kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) zilizopo Mtumba Jijini Dodoma.



Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya akizungumza na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo vya ofisi hiyo (Sera, Uratibu na Bunge) mara baada ya kuwasili katika ofisi hiyo Aprili 8, 2021 Jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Profesa Jamal Katundu akizungumza na Menejimenti ya Ofisi hiyo upande wa Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mara baada ya kuwasili katika ofisi hiyo  Aprili 8, 2021 eneo la Mtumba Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya akizungumza na Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mara baada ya kuwasili na kupokelewa na watumishi hao katika ofisi zao zilizopo Mtumba Dodoma.


Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Ofisi  ya Waziri Mkuu  Bw. Greyson Mwaigombe akifafanua masuala ya Utawala na Rasilimali watu kwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kasper K. Mmuya (kulia) kwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, anaeshughulikia (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda (kushoto)

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Ofisi  ya Waziri Mkuu  Bw. Greyson Mwaigombe akimtambulisha Naibu Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Kaspar Mmuya kwa baadhi ya watumishi wa Ofisi hiyo (Sera, Uratibu na Uwekezaji).




EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.