Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,
Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, amekutana na kufanya
mazungumzo na viongozi wa Plan International – Tanzania, ofisini kwake jijini
Dodoma.
Ujumbe huo umeongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Plan International –
Tanzania Dkt. Mona Girgis, akiwa na Meneja Miradi wa Plan
Interanational Tanzania, Peter Mwakabwale, pamoja na Meneja wa Uchechemuzi wa Plan International Tanzania.
Kupitia kikao hicho, Viongozi hao wa Shirika hilo walipata
fursa ya kueleza kwa kina mipango yao ya kushirikiana na serika kwenye shughuli
wanazozifanya. Wamebainisha kuwa wanayo miradi wanayo tekeleza katika kuchochea
maendeleo ya vijana pamoja na kujumuisha watu wenye Ulemavu kwenye shughuli za
maendeleo.
Katika Mazungumzo hayo Mhe. Mhagama amewahakikishia
kuwa serikali ipo tayari kuendelea kushirikiana nao katika mikakati ya
maendeleo ya vijana na masuala ya watu wenye ulemavu. Amewaeleza kuwa atawaelekeza Wataalamu wa Ofisi hiyo wakutane
na Wataalamu wa shirika hilo ili wapange mipango mikakati ya kushirikiana nao.
Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi,vijana, Ajira na Watu wenye
ulemavu) inaratibu masuala ya Vijana na watu wenye Ulemavu kwa Uhamasishaji wa
vijana, malezi na uwezeshaji wa kiuchumi na kijamii, pia inaratibu masuala ya
Watu wenye Ulemavu kwa kutoa utaalamu na huduma kwa watu wenye ulemavu.
MWISHO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,
Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akiongea na viongozi wa
Plan International – Tanzania, ofisini kwake jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,
Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa Plan International
– Tanzania, ofisini kwake jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,
Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akiongea na Mkurugenzi
Mkazi wa Plan International – Tanzania Dkt. Mona Girgis mara baada ya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano na shirika hilo
walipomtembelea , ofisini kwake jijini Dodoma.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.