Wakuu vitengo vya Ufuatiliaji na Tathmini kwa Mikoa wajengewa uwezo ili kuimarisha ufanisi katika Ufuatiliaji, Tathimini na upimaji wa Utendaji wa shughuli za Serikali katika ngazi ya Mikoa na Halmashauri ili kuweza kujipima katika utendaji wa kazi.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi
wa kikao hicho kilichofanyika Mkoani Singida Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) kutoka Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya
Utendaji wa Serikali (Sehemu ya Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Bw. John
Bosco Quman amesema Ufuatiliaji na Tathmini huratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu
kwa kuzingatia ibara ya 52 (1) (3) inayokasimu Madaraka kwa Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa msimamizi Mkuu wa Shughuli za Serikali
siku hadi siku.
“Ni muhimu kuelewa dhana
mbalimbali zinazohusiana na masuala ya Ufuatiliaji, Tathmini kwa kuzingatia
Upimaji na Utendaji wake, pamoja na kufanya ufuatiliaji wa afua mbalimbali za
Serikali zinazojumuisha; Sera, Mipango, Mikakati, Miradi na Programu
zinazotekelezwa kwenye Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Halmashauri zote nchini,
alieleza Bw, Quman.
Aidha Serikali inaendelea
kukamiikisha Sera ya Kitaifa ya Ufuatliaji na Tathmini Nchini ambayo ipo katika
hatua za Uandishi baada ya kupita katika kamati ya Kitaifa ya uchambuzi wa
Sera.
Bw. Quman amesema, jitihada
zinaendelea katika Mashirika ya Umma pamoja na Makampuni ya Serikali ili kuwa
na Idara za Ufuatiliaji na Tathmini zinazojitegemea kama ambavyo msisitizo
ulivyowekwa katika ngazi ya Mikoa na Halmshauri ili kuhakikisha vitengo hivi
vinajitegemea na kutekeleza majukumu yake.

EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.