Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Mhe. Ummy
Nderiananga ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwaunga mkono Watu Wenye
Ulemavu ili kuendelea kuvumbua vipaji vyao katika maeneo mbalimbali.
Naibu
Waziri ametoa wito huo leo Jijini Dodoma katika Ukumbi PSSSF wakati wa uzinduzi
wa Msimu wa Pili wa Mashindano ya kusoma Quran kwa Watu Wenye Ulemavu
yaliyoandaliwa na Taasisi ya Lulida.
Ameeleza
kwamba, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
itaendelea kushirikiana na Wenye Ulemavu bega kwa bega ili kuhakikisha masuala
mbalimbali yanayowahusu yanapewa kipaumbele.
“Nipo
kwenye hatua ya kupita katika makundi mbalimbali ili kusikiliza changamoto na
kuweka mikakati ya muda mrefu na muda mfupi katika kuzifanyia kazi,” alisema
Naibu Waziri Nderiananga.
Aidha, aliongeza kusema, “nimefurahishwa na
taasisi ya Lulida kwa kuanzisha jambo hili kwa sababu ni sehemu ya kujali Watu
Wenye Ulemavu kuona vipaji vyao na vipawa vyao”.
Naye
Mwenyekiti wa Taasisi ya Lulida Mhe. Hajjat Riziki Lulida ametoa rai kwa vyombo
vya habari kuendeleza upendo na kujikita
katika kuandika habari zenye kujenga misingi ya umoja na ushirikiano kwa jamii.


EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.