Kamati za usimamizi wa Maafa
zatakiwa kuandaa mipango ya dharura itakayoelekeza hatua za kuchukua kwa kila
taasisi na wananchi kwenye maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka
ambapo, mvua zinatarajiwa kuwa chini ya wastani hadi wastani.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene katika
Mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Mjini Dodoma. taarifa ya
utabiri huo inahusu maeneo ya Mikoa ya
Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Kigoma, Arusha, Kilimanjaro,
Manyara, Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na
Pemba.
“kutakuwa na upungufu mkubwa
wa unyevunyevu katika udongo katika maeneo mengi unaoweza kuathiri ukuaji wa
mazao, kusababisha uwepo wa visumbufu vya mazao na magonjwa,” amesema Waziri.
Kina cha maji katika mito,
mabwawa na hifadhi ya maji ardhini kinatarajiwa kupungua hususani katika maeneo mengi ya
yanayotegemea mvua za Vuli hivyo kusababisha upungufu wa maji kwa matumizi
mbalimbali.
“Mlipuko wa magonjwa unaweza
kujitokeza kutokana na upungufu wa upatikanaji wa maji safi na salama.”
Waziri ametoa rai kwa kamati
za usimamizi wa Maafa katika ngazi zote kushirikisha wadau wa maafa kuhakikisha
upatikanaji wa mbegu zinazokomaa kwa muda mfupi pamoja na utunzaji wa chakula
cha binadamu na malisho ya mifugo ikiwemo kupanda mazao yanayokomaa mapema na
kuvuna maji.
“Kamati za usimamizi wa maafa,
zichukue hatua za kuzuia milipuko ya magonjwa yanayoweza kujitokeza kutokana na
upungufu wa upatikanaji wa maji safi na salama ikiwa ni pamoja na Kushirikiana
na sekta za maji na umeme kuweka mipango yao ya tahadhari ili kuhakikisha kuwa
usumbufu unaotokana na ukosefu wa maji na nishati unapewa ufumbuzi mapema”.
Waziri amehimiza Kuimarisha
udhibiti wa maeneo ya hifadhi za wanyama pori ikiwa ni pamoja na kuzuia
muingiliano kadri inavyowezekana;
sambamba na kuainisha na kuandaa rasilimali za usimamizi wa maafa na kila sekta
kushiriki kikamilifu katika eneo lake.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.