Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amewahimiza wadau wa
maendeleo na watu binafsi kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kuchangia
vifaa vya misaada ya kibinadamu wakati wa maafa.
Mhe.
Ummy aliyasema hayo alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua ghala
la kuhifadhi vifaa vya misaada ya kibinadamu wakati wa maafa Kanda ya Kaskazini
lililopo maeneo ya Chekereni, Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani
Kilimanjaro.
Alisema
uungwaji mkono wa serikali kutoka kwa wadau unasadia wananchi kufikiwa na
huduma kwa haraka kutokana na majanga yaliyojitokeza ambayo husabababisha
madhara kama vifo, ulemavu wa kudumu, mali kuharibika pamoja na miundombinu.
“Nitoe
wito kwa wadau na watu mbalimbali ambao wanaguswa kushirikiana na serikali kwa
kutoa vifaa wafanye hivyo pengine ngaji ya Wilaya, Mkoa na hata kijiji ili tuwe
navyo vya kutosha ili yanapotokea tunatoa msaada kwa haraka,” alihimiza Mhe.
Ummy.
Pia
Mhe. Ummy alisisitiza utunzwaji wa magahala hayo hatua itakayosaidia vifaa hivyo
kudumu kwa muda mrefu na kuwa tayari kutumika pindi vinapohitajika katika
maeneo yenye maafa.
Aidha
aliupongeza uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kwa utayari wa kutoa msaada wa
kibinadamu kwa wananchi wanaokumbwa na maafa kwa lengo la kuwasaidia kurejea
katika hali yao ya awali.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa
Kilimanjaro ambaye ni Afisa Mifugo katika Mkoa huo Bwa. James Shao
alisema ghala la Kanda ya Kasikazini linahudumia Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro
na Tanga.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.