Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya ametoa rai kwa watendaji wa
serikali kutunza vizuri vyombo vya usafiri walivyopewa ili viweze kuwasaidia
katika utendaji wa kazi na kudumu kwa
muda mrefu.
Wito huo umetolewa wakati wa
kukabidhi bajaji mbili kwa watumishi wa Ofisi ya Mpiga chapa wa serikali jijini
Dar es saalam katika kuwajengea Mazingira mazuri watu wenye ulemavu ya utendaji
wa kazi.
“Ofisi ya Waziri Mkuu moja ya
jukumu lake ni kuwezesha watu wenye ulemavu kwa kusimamia Sera ya Watu wenye
Ulemavu na Miongozo ya watu wenye Ulemavu”
Akitoa neno la shukrani Bwn.
Ophin Malley ameshukuru serikali kwa
kuwatambua watu wenye ulemavu katika mazingira waliyonayo mahala pa kazi.
“Tunaomba kama itafaa tuweze
kupatiwa baiskeli maalumu ili zituwezeshe kuturahisishia kutoka sehemu moja
kwenda nyingine wakati wa utendaji wa Kazi”
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.