Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera, Bunge Uratibu na Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga, amesema
Watu wenye Ulemavu wa Ngozi wapo Mbioni kunufaika na Mfuko wa Wenye Ulemavu wa
Ngozi kwa kupata mafuta maalum kwa matumizi ya ngozi.
Ameyasema hayo Bungeni Jijini
Dodoma leo katika Bunge la 13 mkutano wa pili kikao cha nne, wakati akijibu
swali la nyongeza lililoulizwa na Mhe. Stella Ikupa Alex (Mb) Viti Maalum CCM
lililohoji ni lini Serikali itatoa
mafuta ya watu wenye ulemavu wa ngozi katika Halmashauri nchini.
Mhe. Nderiananga amesema kuwa,
Serikali inatambua uhitaji wa mafuta kwa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini na
kufafanua kwamba kwa kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia mfuko wa wenye
Ulemavu nchini serikali imetenga fedha maalum
na kuzielekeza Kilimanjaro Catholic Medical Centre (KCMC) ili kuweza
kuzalisha mafuta mengi zaidi na kuyasambaza.
Aliongeza kuwa, kupitia Wizara
ya Elimu, Serikali inasamabaza mafuta hayo ili kuweza kuwafikia wanafunzi wenye
ulemavu wa ngozi na yananunuliwa kama vifaa saidizi.
“Tuna hospitali teule kama
vile Bugando yanafanyika matibabu hayo ya kufanya uchunguzi wa ngozi kwa ajili
ya kutambua aina ya ngozi kwa watoto ili kuwapatia matibabu sahihi na Serikali
ina lengo la kusambaza huduma hizo mpaka vijijini” amefafanua.

EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.