Tuesday, January 4, 2022

Naibu Waziri Ummy Azindua Kisima cha Maji Safi Pemba


Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu(Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kisima cha maji pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kojani na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Hamad Chande yenye kuhudumia wanafunzi wenye ulemavu iliyopo Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba. Uzinduzi umefanyika Januari 04,2022. Kisima hicho kimefadhiliwa na Rehema Foundation kwa kushirikiana na Ofisi za mbunge huyo.


Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga akimtwika ndoo ya maji mmoja wa wanafunzi wa shule ya Msingi ya Mchanga Mdogo Pemba mara baada ya kuzindua rasmi kisima cha maji kinachotarajiwa kutatua changamoto za maji shuleni hapo Januari 04, 2022.

 

Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu)Mhe. Ummy Nderiananga, Mbunge wa Jimbo la Kojani na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Hamad Chande (katikati) na Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Bw. Ussi Khamis Debe wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi ya Mchaga Mdogo Pemba mara baada ya tukio la uzinduzi wa kisima cha maji. Ussi Khamis Debe

 

 Na: Mwandishi Wetu - Pemba, Zanzibar

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuaka ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga amezindua kisima cha maji safi na salama katika shule ya msingi yenye kuhudumia watoto wenye mahitaji maalum ya Mchanga Mdogo iliyopo Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Naibu Waziri huyu amezindua ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi Visiwani humo iliyolenga kutembelea na kujionea shughuli za utekelezaji za masuala ya watu wenye ulemavu Pemba tarehe 04, Januari, 2022.

Akiwa amaeambatana na Mbunge wa Jimbo la Kojani na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Hamad Chande alieleza furaha yake ya uchimbaji wa kisima hicho kitakachosaidia kutatua changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama shuleni hapo huku akishukuru wafadhili waleta huduma hiyo.

“Kipekee niwapongeze Taasisi ya Rehema Foundation na Ofisi ya Mbunge wa Kojani kwa kuchimba kisima na kuonesha umuhimu wa kuleta huduma hii muhimu hasa kwa kundi letu la wenye ulemavu hatua itayosaidia kuboresha mazingira yao na kuchangia ufaulu wao,hii napongeza sana” alisema Mhe. Ummy

Naye Mbunge huyo wa Kojani ambaye pia ni Naibu waziri Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira, aliyaeleza furaha yake ya kukamilika kwa maono hayo huku akisema itasaidia kuchagiza utulivu na kusoma kwa bidii.

“Niwapongeza naibu waziri kuona umuhimu wa kujumuika na jamii yetu na kuzindua kisima hiki, na kisima hiki ni miongoni mwa visima vitano tulivyoomba Rehema Foundation kuchimba na wameshachimba vinne na leo wamehitimisha cha tano, tunawapongeza,”alisema Mbunge.

Kwa upande wake mwakilishi wa taasisi ya rehema Foundation Bw. Mohamed Assa alieleza kuwa, wataendelea kusaidia huduma za kijamii kwa wakazi wa Pemba ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuunga mkono jitihada za serikali na kuwaasa kukitunza ili malengo ya uwepo wa kisima hicho yatimizwe.

Nae mwalimu mkuu wa shule hiyo, Bw.Suleiman Kombo alishukuru jitihada za taasisi na ofisi ya Mbunge huku akiwaasa wanafunzi na wakazi wa maeneo hayo kuhakikisha miradi kama hiyo inalindwa na kutunzwa kwani inasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji kwa jamii kwa ujumla.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.