Saturday, December 14, 2024

MAFUNZO YA UFUATILIAJI NA TATHMNI KWA WIZARA, IDARA ZINAZOJITEGEMEA, WAKALA WA SERIKALI NA MASHIRIKA YA UMMA YAFANYIKA JIJINI TANGA

 


Afisa Muandamizi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw.Charlton Charles Meena amewataka washiriki wote wa mafunzo ya awamu ya kwanza ya ufuatiliaji na tathmni yaliyoshrikisha wizara, idara zinazojitegemea, wakala wa serikali na mashirika ya umma kuwa na mundelezo mzuri wa mafunzo ya awamu zote tatu ili kuweza kujipambanua vizuri katika utendaji wa kazi zao.

Kauli hiyo ameitoa Jijini Tanga wakati wa kuahirisha mafaunzo ya ufutiliaji na tathimini yaliyofanywa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kupitia kitengo chake maalumu cha ushauri wa kitaalam na kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) pamoja na washirika wengine Ofisi ya Msajili wa Hazina, yaliyofanyika katika ukumbi wa New Kiboko Hall Jijini Tanga kwa muda wa siku tatu.

Ameeleza kwamba Mafunzo yameshirikisha watumishi wa umma zaidi ya 200, na yamewawezesha washiriki kujifunza kutofautisha na kutumia ipasavyo aina tofauti za Ufuatiliaji na Tathmini, kuamua jinsi ya kufuatilia na kutathmini miradi, mipango ya kimaendeleo na sera ikiwa ni pamoja na kuweka bayana matokeo muhimu katika ngazi ya programu kwa kutumia mfumo wa kimantiki (Logical Framework) au miundo ya nadharia ya mabadiliko (Theory of Change).

Bw, Meena, alisema “mafunzo yamelenga kuunda viashiria sahihi (SMART), kwaajili Ufuatiliaji na Tathmini, kutumia zana mbalimbali za Ufuatiliaji na Tathmini kwaajili ya ukusanyaji na uchanganuzi wa takwimu, kubuni na kusimamia Tathmini kwa kutumia kanuni za Kiafrika za Tathmini na vigezo vya OECD-DAC na kuandaa ripoti bora za Ufuatiliaji na Tathmini kwaajili ya matumizi ya Serikali, Idara, Wizara, Mashirika na Wakala za Serikali.

Aidha kutokana na umuhimu wa mafunzo hayo, Chuo Kikuu Huria kitaendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, pamoja na Msajili wa Hazina kuandaa awamu nyingine ya mafunzo ya awamu ya kwanza ili kuweza kuzifikia baadhi ya Wizara, Idara zinazojitegemea, mashirika na wakala za serekali ambazo zilishindwa kuleta watumishi kwenye awamu hii ya kwanza ya mafunzo.

“ni vyema kujenga uelewa wa pamoja  sasa,  kwasababu kutakua na awamu ya pili na ya tatu ambazo zitawezesha  watumishi kubobea katika eneo la Ufuatiliaji na Tathmini wa shughuli za Serikali na hivyo kuboresha utendaji kazi wa serikali na utoaji huduma kwa wananchi,” alibainisha.

 


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.