Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt Jim Yonazi
amempongeza Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Anderson Mutatembwa
kwa Kuteuliwa kuwa Balozi.
Dkt. Yonazi Ametoa pongezi
hizo wakati akimuaga Mhe. Balozi Mutatembwa na Kumakaribisha Naibu katibu Mkuu
mpya Dkt. James Kilabuko.
Dkt. Yonazi amempongeza Balozi
Mutatembwa kwa kufanya kazi ya ushauri kwa utulivu aliyotokana hekima
aliyojijengea na kujaliwaa na Mwenyezi Mungu kuwa nayo “Na ndiyo maana Mhe.
Rais ameweza kukuamini na kukuteuwa katika nafasi ya Ubalozi ili uweze
kumuwakilisha yeye pamoja na Nchi katika maeneo ambayo atakayoona inampendeza.”
Alifafanua
Aliendelea kusema kuwa, nafasi
ya ubalozi ni nafasi nyeti na adhimu sana na ni fursa inayopatikana kwa watu
wachache sana, “umepata fursa nyeti sana ya kuitumikia Taifa naamini utaendelea
kufanya kazi kama ambavyo umekuwa ukifanya hapa na utakaoenda kufanya nao kazi
watafaidika na kufurahia kama tulivyo faidika sisi.” Alibainisha Dkt. Yonazi
Akimkaribisha Naibu Katibu
Mkuu mpya Dkt. James Kilabuko, Katibu Mkuu Dkt. Yonazi alisema Ofisi ya Waziri
Mkuu ni Ofisi yenye majukumu mazito yenye watumishi wachapakazi wenye kutizama
tija katika utendaji wa majukumu yao ya kila siku.
Naibu Katibu Mkuu, Dkt. James
Kilabuko Alimshukuru Mhe. Rais kwa kumteuwa katika nafasi hiyo na kuona kwamba
anaweza kumsaidia Katibu Mkuu Kiongozi katika nafasi hiyo, aliendea kusema kuwa
anategemea kupata ushirikiano kutoka kwa Watumishi na Menejimenti ya Ofisi ya
Waziri Mkuu katika kumsaidia Katibu Mkuu Dkt. Jonazi kiutendaji na kufikia
malengo yanayotegemewa na mamlaka za juu.
Kwa Upande wake Mhe. Balozi
Anderson Mutatembwa, alimshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea Kumuamini na kumteuwa katika nafasi
hiyo.
Aidha, Ameishukuru Menejimenet
ya Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu pamoja na watumishi wa Ofisi
hiyo kwa ushirikiano waliomupatia wakati wa utekelezaji wa majukumu yake
ofisini hapo, aliendelea kusema kuwa ni sehemu ambayo atapakumbuka kwani amefanya
kazi kwa amani na Utulivu wa hali ya juu.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.