Tuesday, November 29, 2022

SERIKALI YALENGA KUIMARISHA USAWA MAPAMBANO VIRUSI VYA UKIMWI

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amepongeza Tume ya kudhibiti UKIMWI, Wizara ya Afya na Wizara ya TAMISEMI katika Mkakati wa kupambana na Ukimwi kama janga la kitaifa.

Hayo yamesemwa Waziri na Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene Jijini Dar es saalam, wakati wa uzinduzi wa taarifa ya hali ya UKIMWI duniani yenye Kauli Mbiu inayosema Dangerous Inequalities iliyotolewa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia Ukimwi Duniani UNAIDS Bi, Winnie Byanyima.

“Serikali imedhamiria kuweka usawa wa kijografia usawa kimazingira usawa kati ya watoto na wakubwa na usawa wa kiuchumi ili kuhakikisha watu wote wanapata huduma sawa ili wasiathirike na wale walio athirika wapate huduma za matibabu lakini pia huduma sawasawa kuhakikisha wanaendesha maisha yao.”

Akitoa taarifa hiyo Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia Ukimwi Duniani UNAIDS Bi, Winnie Byanyima amesema Tanzania imejitahidi kupunguza Ongezeko la Maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI kila Mwaka kwa miaka kumi mfululizo.

“Tanzania Imejitahidi kupunguza vifo vinavyosababishwa na UKIMWI na imekuwa ikifanya vizuri katika mapambano dhidi ya virusi vya UKIMWI.”

 


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.