Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia na (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga ametoa
rai kwa wananchi, Taasisi na Wizara kuunga mkono juhudi za Serikali kwa
kutembelea vivutio vyetu vya utalii wa ndani.
Wito huo umetolewa wakati Viongozi
na Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake, walipotembelea Mamlaka ya
hifadhi ya Ngorongoro baada ya kutoka katika Mkutano wa Mazingativu Mkoani
Arusha.
"Tunamshukuru na
kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa alizozifanya
katika sekta ya utalii kupitia filamu ya Royal tour," alibainisha.
"Tumefika Ngorongoro na
tumejionea wageni wamefurika wamekuja kujionea vivutio vya utalii."
Alisisitiza.
Aidha, alitoa shukrani nyingi
Kwa Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa
kwa kutoa ruhusa ya kutembelea eneo hilo la Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.
Aliongeza Kwa kusema kuwa, ziara
hiyo imeimarisha upendo, uongozi na urafiki kati ya viongozi na watumishi na
itaongeza hari ya utendaji kazi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia na (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim
Yonazi amesema, ziara hiyo ni Maelekezo ya Mhe. Waziri Mkuu kwa lengo la
kuhakikisha kwamba tuna viongozi wa kusimamia Sera na wanalifahamu eneo la
utalii wanaloliratibu Sera zake katika Serikali.
"Tumekuja kuona Mazingira
halisi ya Utalii pamoja na Mazingira halisi ya Utendaji kazi, Tumeona Utalii
umekuwa kwa kiasi kikubwa wageni ni wengi na sisi kama Serikali tunawajibu wa
kuhakikisha tunaweka sera bora za kuwasaidia wageni kuendelea kuja nchini,"
Alisisitiza
Aliendelea kusema kuwa, eneo
la Ngorongoro ni zuri linavutia na Watanzania wana fursa ya kuja kujionea.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.