Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Mhe. Jenista Mhagama ameitaka Idara ya
Ufutiliaji na Tathimini ya Utendaji wa Shughuli za Serikali kushirikiana na
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini, (TAKUKURU) katika kutumia
Mfumo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathimini ya Utendaji wa Shughuli za
Serikali, ili kuweza kuondoa upendeleo, Rushwa na kutoa huduma bora kwa
wananchi katika utendaji Serikalini.
Kauli hiyo ameitoa leo Jijini
Dodoma alipokuwa katika kikao kazi cha Mapitio kilichohusisha Wakurugenzi, wa
Idara na Wakuu wa vitengo wa Ofisi hiyo ambapo, Mamlaka ya Serikali Mtandao
imefanya wasilisho la Mfumo wa Taifa wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa
shughuli za Serikali.
Waziri Mhagama Alisema kuwa, eneo
la Ufuatiliaji na Tathmini ni eneo ambalo haliwezi kukwepeka “Leo Tumekutana
hapa tumefanya kazi nzuri ya kufanya mapitio na kuangalia ramani hii ambayo
inaanza na kuwa na mfumo wa Ufuatilia na Tathmini Nchini, kama nyenzo muhimu
sana ya Utendaji kazi ndani ya Serikali.” Alisisitiza
Aliendelea kusema kuwa, Mfumo
huu utasaidia kushauri namna ya kujipanga na namna ya kufanya kazi ndani ya
Serikali ,“Mfumo huu utusaidie kuchakata
kila kitu na kutusaidia kupata matokeo sahihi kwa jambo sahihi na shughuli
sahihi, katika kupima utendaji kazi na matokeo yake.” Alifafanua.
Aidha, Alisema pia kwa Mujibu
wa Sheria kuna Taasisi ambazo zimekasimiwa majukumu ya kufanya, zinazofanana na
Idara hii akitolea mfano Tume ya Taifa ya Mipango, na kusema ni lazima kukutana
na Tume hii ya Mipango ili kila mtu afanye kazi kwa kufuata Sheria na
Kuzingatia Mifumo iliyopo. “Ni lazima kufanya Tathmini na Ufuatiliaji wa
matumizi sahihi ya fedha katika Utekelezaji wa Miradi na utendaji wa shughuli
za Serikali, eneo hili kwenye mfumo liwekwe vizuri na liweze kutusaidia,”
Alisema.
Kwa Upande wake Naibu Waziri
wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga, Alisema
Mamlaka ya Serikali Mtandao (Ega) imefanya wasilisho zuri lenye kutoa muelekeo
wa Utendaji wa Shughuli za Serikali Utakaosaidia Ofisi ya Waziri Mukuu kuratibu
vizuri shughuli za utendaji Serikalini katika kuripoti na kufanya Tathmini.
Akiongea baada ya wasilisho
hilo, Mkurugenzi wa Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Shughuli za
Serikali, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bi. Sakina
Mwinyimkuu alisema, Idara yake Itajitahidi kufuatilia kwa Ukaribu ukamilishwaji
wa mfumo huo kwa wakati, ili Taasisi za Umma ziweze kushirikishwa na mfumo
uweze kufanya kazi kwa wakati kwenye upimaji wa Utendaji wa Shughuli za
Serikali.
Awali, Akiongea katika kikao
kazi hicho, Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA cha Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge
na Uratibu) Bw. Innocent Mboya alisema, Amepokea maelekezo ya kukamilisha mfumo
huo ndani ya mwaka huu wa fedha 2023/2024.
“Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Kushirikiana na Mamlaka
ya Serikali Mtandao, tunaahidi kwamba ndani ya hizi wiki mbili, tutakuwa
tumeandaa mpango kazi ambao utatupeleka kwenye ramani na utelekelezaji wa mfumo
huu, na ndani ya miezi mitatu tutakuwa tumekamilisha mfumo huu kwa kufuata
matakwa na maelekezo ya Serikali.”
Alisisitiza
Walisisho hili ni Sehemu ya
Utekelezaji wa Maelekezo ya Mhe. Waziri Mhagama aliyoyatoa katika kikao cha
mazingativu kilichofanyika Mkoani Arusha Mapema Mwezi huu.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.