Saturday, December 2, 2023

“WAHITIMU CHUO CHA BIBLIA MUWE MABALOZI WAZURI WA KUSIMAMIA MAADILI” WAZIRI MHAGAMA


 Wahitimu wa Chuo cha Biblia cha Evengelism Church wameaswa kuwa askari wazuri wa vita dhidi ya mmomonyoko wa maadili ambao unaendelea kushamiri katika jamii zetu hususani kwa vijana.

Wito huo umetolewa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe, Jenista Mhagama wakati wa mahafali ya 83 ya chuo hicho yaliyofanyika, Sakila Katika wilaya ya Meru Mkoani Arusha.

Waziri aliwaambia wahitimu hao kwamba maendeleo ya taifa letu yanategemea sana nguvu kazi na nidhamu ya kazi, japokuwa nchi yetu haiegemei upande wowote katika maswala ya dini, lakini sehemu kubwa ya watu wake wanaamini katika dini kupitia madhehebu mbalimbal

 “ni muhimu mkawe mabalozi wazuri katika vita hii na mkashirikiane na viongozi wengine wa dini na Serikali ili kwa pamoja tuhakikishe tunalilinda taifa letu dhidi ya upotofu huu wa maadili” alibainisha.

Aidha, aliwasihi kuendelea kuliombea taifa amani, utulivu, upendo na mshikamano ili kulijenga taifa.

Waziri ametumia maandiko matakatifu, katika Injili ya Matayo (Sura ya 5:13-16) ambayo yalisema, nami pia niwasihi popote mnapokwenda, mkawe chumvi ya dunia na kamwe msipoteze ladha ya chumvi lakini pia mkawe mwanga wa ulimwengu ukaangaze mbele ya watu ili wayaone matendo yenu mema wamtukuze baba yenu aliye mbinguni.

“Sina shaka kwamba, wote mkitoka hapa mtakwenda kutekeleza jukumu la kichungaji na kufundisha watu kwa upendo, uaminifu na kuwaongoza katika kweli maana huo ndio wito mlioitiwa,” alifafanua

Kwa upande wake Dkt. Eliud Issangya, Askofu Mkuu wa International Evengelism Church na Mkuu wa Chuo cha Biblia Sakila; alisema wahitimu wa chuo cha Biblia wanapaswa  kwenda kuweka mkazo wa kufundisha maadili kwenye jamii.

“Msambaze maandiko kwa kulenga maadili na si kwa kutafuta mali, bali watu waweze kuishi kwa kuthaminiana na wawe watu wenye hekima,” alihimiza

Awali muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe, Joshua Nassari Mkuu wa wilaya ya Monduli alisema serikali ya mkoa wa Arusha itaendelea kutoa ushirikiano wa kiroho kwa chuo hicho cha Biblia na madhehebu mengine.

“Jamii yetu imekuwa ikipitia changamoto kubwa za mabadiliko ya kimadili na kitamaduni hivyo tujikite katika kufundisha maadili mema ya kitanzania na madili mema ya Imani ili tuwe na jamii iliyostaarabika,”alihimiza


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.