Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama amesema misaada yote
inayotolewa na wadau mbalimbali itawafikia walengwa walioathirika wa poromoko
ya matope kutoka Mlima Hanang’.
Kauli hiyo ameitoa wakati
alipozindua zoezi la ugawaji wa vifaa vya msaada wa kibinadamu kwa familia 205 zilizoweka
makazi ya muda katika shule ya sekondari ya Katesh iliyopo katika Halmashauri
ya Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.
Chochote tutakachokipata
tutakigawa kwa walengwa kwa sababu hili zoezi ni sehemu ya majukumu yetu na
tutalitekeleza kwa uaminifu mkubwa.
“Atakayefanya ubadhilifu wa
aina yoyote, serikali haitakuwa na uvumilivu naye, tutachukua hatua,”
alibainisha Waziri
Serikali ipo pamoja na nyie,
tunajua maswahibu mliyoyapata: wengi wenu mlishapiga hatua za kimaisha, lakini
janga hili limeturudisha nyuma, kikubwa tuwe na moyo wa subira kwa mwenyezi
Mungu kwa kuendelea kutulinda.
“Kazi kubwa ilikuwa ilikuwa ya
kukabiliana na janga lilipotokea na hatua ya pili ni kurudisha huduma za
kijamii na miundo mbinu ya mawasiliano, katika hali ya kawaida,” alifafanua
katika hatua nyingine waziri
Mhagama ameishukuru shirika la umeme TANESCO kwa kurudishia transfoma 76
zilizokuwa zimeharibika na nguzo zaidi ya 60 na hivyo kusaidia kijiji cha
Gendabi kilichoathirika na Maporomoko.
“Niwaombe sasa muanze kufanya
ufuatilaiji wa nyumba zote zilizokuwa zinapata nishati ya umeme ili wananchi
wandelee kupata huduma hiyo alisema,” Waziri.
Awali Luteni Kanali Selestine
Masalamadu Mkurugenzi Msaidizi idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri
Mkuu, amesema kila familia itapata magodoro 3; masufuria 5, sabuni za miche
pamoja na sabuni za unga na nguo za watoto.
Kwa upande wa Bi, Betha Mmari
Mwananchi aliyepata adha ya mafuriko ameishukuru serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, na kwa Mama Samia kwa Kujali.
“Tunaomba muendele kutuhudumia
katika kipindi hiki kigumu kwetu na msituache” alisema
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.