Serikali imesema zoezi
la ufunguaji wa mitaa katika mji wa Kateshi limefika 85% na mkazo mkubwa
umewekwa katika kutoa udongo kwenye vipenyo vya vya mtaa kwa mtaa na nyumba kwa
nyumba.
Kauli hiyo imetolewa
na Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista
Mhagama katika mahojiano maalumu aliyoyafanya na shirika la utangazaji la Taifa
TBC leo Hanang Manyara
Waziri alisema katika
zoezi hilo malori makubwa zaidi ya 30 yalisaidia kutoa tope lenye mawe miti
pamoja na udongo, katika barabara kuu ya Katesh Singida.
“Malori yenye uwezo wa
kubeba magunia 130 yamefanya safari zaidi ya 400 ya kutoa Tope kutoka kwenye
viunga vyote vya Mji wa Katesh,” alibainisha.
Waziri amefafanua
kwamba, vifaa tulivyonavyo haviwezi kuingia kwenye vipenyo vya mtaa kwa mtaa au
nyumba kwa nyumba na hivyo tunalazimika kutumia nguvu kazi, na tunafanikiwa.
Halikadhalika
tunafikiria kushirikisha wananchi kujitokeza kusaidia zoezi la uondoaji wa tope
hasa kwenye hifadhi ya barabara ili tuweke hali katika usalama zaidi.
“Tunafanya tathimini
na kuendelea kuchukua tahadhari mvua nyingine ikinyesha, ikiwa ni pamoja na
kurudisha mto uliopokea mawe na matope ambao njia yake ilifunga na kutengeneza
mapito mengine,”alifafanua.
Kwa upande wake Mkazi
wa Katesh, Bi, Halima Rashidi amesema Mawe na tope yaliyoletwa na Mlima Hanang
yaliathiri kwa kiasi kikubwa miundo mbinu na makazi ya watu.
“Msaada wa serikali
umekuja kwa wakati na haraka, watu wana moyo wa kufanya kazi kwa sababu
jitihada zao zimeokoa maisha ya watu na mali,” alibainisha
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.