Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama ameelekeza watendaji wa Idara ya Menejimenti ya Maafa katika ofisi hiyo kuhakikisha wanaweka utaratibu wa kimfumo ili misaada yote iingie kwenye mfumo rasmi ili iweze kuwafikia wale waliokusudiwa.
Ametoa kauli hiyo wakati
akipokea vifaa vya msaada wa kibinadamu vilivyowasilishwa na wadau mbalimbali
kusaidia wahanga wa maafa yaliyotokana na maporomoko ya mawe na tope kutoka
mlima Hanang Mkoani Manyara.
Waziri Mhagama alisema Serikali
imepokea misaada hiyo huku akishukuru kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwahakikisha kuwa misaada
hiyo itasimamiwa kwa ukaribu ili kuhakikisha inaleta tija kwa wahusika.
“kipekee niwapongeze na kuwashukuru
sana kwa namna mlivyoguswa na kuungana na Serikali katika kuwanusuru ndugu zetu
waliopatwa na maafa haya, Hanang Tunawashukuru sana,” alisisitiza
Alitumia nafasi hiyo kutoa
onyo kwa yeyote atayejaribu kufanya utapeli au kujinufaisha isivyo halali
katika kipindi hiki.
“Tumewaonya matapeli wasije
wakathubutu kutengeneza akaunti za utapeli kwa sababu tutawakamata na serikali
itachukua hatua kali za kisheria,” alibainisha
Waziri Mhagama alitumia nafasi
hiyo kueleza umma kuwa Serikali imetoa akaunti sahihi ya kutuma michango ya
kifedha kwa ajili ya masuala ya maafa ambapo ni kwa akaunti ya bank yoyote ya
ndani au nje ya nchi.
“Kwa ajili ya kukabiliana na
maafa ya Katesh itatumika Akounti ya
Mfuko wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa (National Disaster Management Fund
Electronic Account) Na. 9921151001 kwa kuandika neno maafa likifuatiwa jina la
Wilaya ya Hjanang’.
Halikadhalika alitoa rai kwa
watumishi watakaohusika na misaada itakayotolewa kuhakikisha wanafanya kazi kwa
uaminifu ili misaada iwafikie walengwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kupitia Chama Cha Mapinduzi
Mhe.Mary Chatanda alisema anatoa pole kwa niaba ya Umoja wa wanawake Tanzania
kwa tukio hilo lenye kuleta majonzi na huzuni kubwa kwa wana Hanang’, jamii na Taifa kwa ujumla.
Tunashukuru wafadhili
mbalimbali wameweza kutuchangia, tumekuja na Mablanketi 120, mashuka 300,
mashuka ya kimasai 500, madira ya kuvaa wanawake 520, kanga 1000, katoni za
sabuni na mafuta ya kupaka,” alisema
Aidha alitoa rai kwa jamii,
wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kusaidia ili kuwapa nafuu waliofikwa na
maafa hayo.
“Wabunge wetu wa viti maalum nao wamesaidia kuchangia kupitia kwa Ktibu wao wa wabunge na fedha hizo tutawasilisha baadae,” alieleza Mhe. Chatanda
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.