Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa
Serikali yatakiwa kuweka mifumo mizuri ya usambazaji wa nyaraka za wazi kwa
wananchi kupitia mifumo ya kidigitali na hata kwa mifumo ya nyaraka ngumu ili
wananchi wanufaike na taarifa hizo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe William Lukuvi alipofanya
ziara katika Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Jijini Dodoma t ambapo amejionea maendeleo ya ujenzi na ufungaji wa mitambo mipya ya
uchapishaji wa nyaraka za serikali.
Amesema, nyaraka nyingi na
muhimu huchapwa kwenye Gazeti la Serikali hivyo mkiongeza uelewa kwa wananchi juu
ya namna ya kulipata Gazeti la Serikali inarahisha taarifa hizo muhimu kufikia walengwa.
“Tunaweza kufanya jitihada
hizi za kusambaza taarifa la Gazeti la Serikali kupatikana katika shule kwa
njia za kidigitali kupita mifumo ya computa ambazo zimeanza kutumika katika
utoaji wa elimu ili wanafunzi waweze kuzipata,” alifafanua
Nitoe rai kwa Idara ya Mpiga
Chapa Mkuu wa Serikali hasa kwenye nyaraka ambazo ni za wazi fanyeni
uelimishaji ili taarifa Magazeti ya Serikali ziweze kuwafikia wananchi.
“Tunaamini Serikali kwa
kununua mitambo hii ya kisasa itasaidia Watendaji wa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu
wa Serikali kujiweka sawa kimafunzo na maadili ili utunzaji wa nyaraka na siri
uzidi kuimarika,” alisisitiza
Hivyo basi Idara ya Mpiga
Chapa Mkuu wa Serikali inaendelea kuwa mhimili
Mkuu wa Serikali kwa miaka yote katika uchapishaji wa nyaraka za Serikali hasa
zinapokuwa nyaraka nyingi na nyeti na zinahitajika kwa uharaka.
Kwa upande wake Mpiga Chapa
Mkuu wa Serikali Bw. George Lugome amesema wanatengeneza mfumo wa mtandao ambao
utamsaidia mteja kujaza taarifa zake na kufanya malipo kwa njia ya mtandao na
tangazo kutoka katika gazeti la serikali.
Ameongeza kusema “mfumo wa
mtandao hauhusiki taarifa za mirathi ambazo uwasilishaji wake unahitaji Mhusika
kuleta vielelezo vyake vya uthibitisho kwa mujibu sheria.”
Mpiga Mchapa amesema, kwa
uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika ununuaji wa mashine za kisasa
utasaidia katika kuongeza uzalishaji na kuongeza maduhuli ya Serikali.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.