Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi amesema Tanzania imebahatika
kuongozwa na viongozi wanaojali utu na kutanguliza maslahi ya taifa mbele hivyo
tunamshukuru Mungu kwa kuwafanya sehemu ya historia kwa sababu taifa
linaendelea kushuhudia mazuri waliyofanya kwa ajili ya nchi.
Waziri
Lukuvi ametoa kauli hiyo wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ibada ya Misa Takatifu ya kumuombea aliyekuwa
Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli iliyofanyika Kanisa
Katoliki la Mt. Yohaba Maria Muzevi Chato.
“Leo
tunadhimisha miaka Minne tangu tondokewe na mpendwa wetu Hayati Rais wa Awamu
ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli, kwa hali ya kibinadamu si rahisi kusahau
kumbukumbu ya kuondokewa na mpendwa wetu kwa jamii inayomfahamu na kujumuika
naye katika maswala mbalimbali ya kitaifa”.
Aidha,
amebainisha kuwa, Hayati Ally Hassani Mwinyi, Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania wakati wa uhai wake aliwahi kusema, “maisha ya
mwanadamu ni hadithi tuu, basi ewe ndugu yangu kuwa hadithi nzuri kwa wale
watakaosimuliwa”, hii inamaanisha viongozi waliopita wameishi vyema na ndio
maana tuna ujasiri wa kusimulia yaliyomema katika kumbukizi zao na kuendelea
kusimulia yaliyofanywa na Hayati Dkt, John Pombe Magufuli.
“Hayati
Dkt, John Pombe Magufuli alikuwa kiongozi aliyejali watu na rasilimali za nchi
yake na mchamungu hivyo tutaendelea kushirikiana na familia katika kumuenzi,
kumuombea na kutangaza mema aliyoyafanya katika jamii na kama baba wa familia
na kiongozi wa taifa letu,” alieleza.
Aidha,
Waziri Lukuvi amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan amekuwa karibu na familia tangu wakati wa uhai wa mtangulizi wake
Hayati Dkt. John Pombe Magufuli mpaka sasa.
“Upendo
na ukaribu wake kwa familia umedhihirishwa kwa mambo mengi, mambo mengine
tunayaona na yapo mengine familia wanayajua na sisi wengine hatuwezi kuyaona
ndio maana katika matukio muhimu kama haya familia imekuwa ikimualika moja kwa
moja, na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani amekuwa akiitikia mialiko hiyo kwa
kushiriki yeye mwenyewe au kutuma miongoni mwa wasaidizi wake kuja
kumuwakilisha pale anapokuwa na majukumu mengine ya kitaifa” alisema Waziri
Lukuvi.
Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi amesema Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania aliyeshika kijiti ameendeleza yale yote yaliyoanzishwa na Dkt. Magufuli na tumeshuhudia miradi mingi ikikamilika, mingine ikiwa katika hatua ya kuelekea ukamilifu na miradi mingi imeanzishwa kwa mwenendo ule ule na fikra zilezile kwa slogani yake kazi iendelee.
“Ni
adhima ya Mhe. Rais Dkt, Samia Suluhu kuwaenzi viongozi wakuu wa kitaifa
waliomtangulia na hatuna budi kuwaenzi viongozi hao kwa vitendo katika utendaji
washughuli zetu, hivyo ni wasihi tuendele kumuombea ndugu yetu Hayati, John
Pombe Magufuli na familia yake ikiongozwa na mama Janeth Magufuli”
“Tuendelee pia kumuombea Rais
wetu wa Awamu ya Sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuliongoza
taifa kwa utulivu na amani kama tunavyoshuhudia sasa Tanzania imetulia kwa
sababu Mkuu wa Nchi anafanya kazi kwa niaba ya Watanzania wote,” alibainisha.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe.
Martin Shigela amemshukuru mama Janeth Magufuli kwa jinsi alivyoweka utaratibu
wa kumkumbuka Hayati John Pombe Magufuli lakini pia amemshukuru Mhe. Rais Dkt.
Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza misingi ya amani na utulivu.
“Tuendelee
kumuombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aendele kuliongoza taifa kwa utulivu,
amani na maendeleo kama tunavyoshuhudia sasa Tanzania ikiwa imetulia,”
alihimiza
Nae, Askofu wa Jimbo katoliki
Rulenge Ngara Mhashamu Severine Niwemugizi amesema Kanisa Katoliki lina
utamaduni wa kuwakumbuka marehemu wote, ambao pia ni desturi ya kujifunza
kutokana na maisha yao.
“Tunajua
Hayati Dkt, Magufuli alipenda nidhamu katika utumishi wa umma na kuwajibika
ikiwa ni pamoja na kukata mambo mabaya rushwa, unyanyasaji na uonevu hivyo
tuandike kitabu chetu tukiwa tunaishi, ili tukimaliza kuandika kiwe na kurasa
zenye mambo mazuri tuweze kujifunza na yale mambo mabaya tuachane nayo,”
alieleza.
Akizungumza
kwa niaba familia Bi, Jesca Magufuli, amemshukuru kwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuunga mkono na
kudumisha maono ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
“Miaka
minne iliyopita alipotembelea hapa Chato alituahidi kama familia kwamba hata
tuacha na leo tunashuhudia uaminifu wake katika kutekeleza ahadi zake,” alisema
Bi. Jesca.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.