Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu wamehimizwa kuratibu vyema taarifa za utekelezaji wa Serikali ya Awamu ya Sita na kuzisemea kazi hizo kwa wananchi ilia wapate uelewa wa uhakika wa miradi ya maendeleo iliyofanywa na Serikali katika maeneo yao.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uaratibu)
Mheshimiwa William Lukuvi wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi la
Ofisi ya Waziri Mkuu, katika Ukumbi wa Ngome Jijini Dodoma.
Ameongeza
kusema Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu wana majukumu makubwa hivyo wanapaswa
kuwa kioo katika utekelezaji wa kazi vizuri na usimamizi wa shughuli za
Serikali ili waweze kuratibu taarifa za mafanikio kwa wananchi.
“Tunalo
jukumu la kuwaambia wananchi kazi zilizofanywa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu
Hassan katika kipindi chake cha uongozi na kwa kuzipambanua vizuri ikiwa ni
sehemu ya uratibu ili wananchi wazijue kwa uhakika huko waliko,” alieleza
Waziri.
Ili
tuweze kuratibu lazima majukumu yaliyo ndani ya Ofisi yetu yaweze kusimamiwa
vizuri sana kwa kuwa mfano katika idara zetu ili tuweze kusimamia idara na
taasisi zilizo nje vizuri.
Amefafanua,
Waziri Mkuu anaamini kwamba watendaji wa Ofisi yake wapo na wanamsaidia katika
jukumu kubwa la kuratibu shughuli zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
“Nikupongeze
tena Katibu Mkuu Dkt. Yonazi kwa usimamizi mzuri na timu ya menejimenti ya
Ofisi ya Waziri Mkuu, tuendele kushirikiana katika kufanya kazi lakini
niwapongeze Wakuu wa Idara na Vitengo nimewatembelea mnafanya vizuri sana,”
alisema Waziri.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Dkt. Jim
Yonazi ameshukuru Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Naibu Waziri wa
Ofisi hiyo kwa miongozo mizuri wanayotoa ili kuweza kutimiza majukumu ya kila
siku.
“Viongozi
wetu Wakuu wanafahamu kazi ambazo tumekuwa kukizifanya na kwa kupitia nyie
tunaomba mtufikishie salamu za shukrani kwao,” alieleza
Naye
Msaidizi wa Katibu wa (TUGHE) Mkoa wa Dodoma Bi, Maisha Mbilla amesema
wanafahamu kwamba watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)
wanafanya kazi kwenye mazingira mazuri na wanapata stahiki zao vizuri, na
kuupongeza uongozi wa Ofisi hiyo.
“Hii
inatutia faraja na moyo na tuna wajibu kama Chama Cha Wafanyakazi wakuongea na
watumishi ili waendelee kufanya kazi kwa kufuata sheria kanuni na taratibu
pamoja na miongozo ya Utumishi wa Umma,” alihimiza
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.