Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. James Kilabuko, ameongoza kikao cha
Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali kilichofanyika leo jijini Dodoma kwa lengo
la kujadili namna bora ya kuimarisha uendeshaji wa Tanzania Safari Channel
chini ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Akizungumza katika kikao
hicho, Dkt. Kilabuko amesema chaneli hiyo imekuwa nyenzo muhimu ya kuitangaza
Tanzania kimataifa kupitia vivutio vya utalii vilivyopo nchini, hivyo ni muhimu
kwa taasisi zote za serikali kushirikiana katika kuiendeleza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi
Mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba Chacha, akiwasilisha taarifa kuhusu chaneli hiyo,
ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa kusaini sheria mpya ya TBC, ambayo imefungua milango ya maboresho ya
kiutendaji na kuimarisha utoaji wa huduma kwa umma.
Chaneli ya Tanzania Safari
Channel imekuwa chombo mahsusi cha kuitangaza Tanzania kama nchi yenye vivutio
vya kipekee duniani, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kimkakati kukuza sekta ya
utalii.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.