Maofisa waandamizi kutoka
Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Zambia wametembelea Mji wa
Serikali Mtumba, jijini Dodoma, kwa lengo la kujifunza namna Tanzania
ilivyofanikiwa kutekeleza mradi mkubwa wa kitaifa wa kuhamishia shughuli za
serikali katika mji huo.
Wakiwa katika ziara hiyo,
maofisa hao walipokelewa na Mratibu wa Ujenzi wa Mji wa Serikali, Bw. Noel
Mlindwa, ambaye alieleza kuwa Tanzania imeweka historia kwa kuanzisha na
kutekeleza kwa mafanikio makubwa ujenzi wa mji wa serikali, chini ya uongozi wa
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Bw. Mlindwa alifafanua kuwa
mji huo umejengwa kwa kuzingatia mipango bora ya kisasa, usimamizi makini wa
rasilimali na matumizi ya teknolojia, hali iliyowavutia wageni hao kutoka
Zambia.
Kwa upande wao, maofisa wa
Zambia waliipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua kubwa ilizopiga na
walisisitiza kuwa Mji wa Serikali Dodoma si tu ni kielelezo cha maendeleo, bali
pia ni kivutio cha kiutalii na mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine barani
Afrika.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.