Naibu Waziri wa Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Ummy Nderiananga, ameshiriki katika
hafla ya uzinduzi wa mfumo wa anuani za makazi, unaolenga kutoa huduma ya barua
ya utambulisho wa mkazi kwa njia ya kidijitali.
Uzinduzi huo umefanyika leo
katika Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar, ukiongozwa na Mgeni Rasmi, Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
Akizungumza katika hafla hiyo,
Mhe. Ummy amepongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan, pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa jitihada zao za kuimarisha huduma za kijamii
kupitia mifumo ya kidijitali.
"Niwapongeze kwa
kuendelea kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi kwa urahisi zaidi kupitia
teknolojia. Mfumo huu utarahisisha utambuzi wa makazi na uboreshaji wa utoaji
wa huduma mbalimbali serikalini," alisema Mhe. Ummy.
Aidha, amezipongeza wizara
zote za kisekta kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano wao uliowezesha utekelezaji wa mfumo
huo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.