Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. James Kilabuko, amesema Serikali
itaendelea kushirikiana kwa karibu na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo
(IFAD) katika utekelezaji wa miradi ya kilimo na uvuvi nchini.
Ametoa kauli hiyo Jijini
Dodoma wakati wa kikao na ujumbe wa IFAD waliopo nchini kufuatilia utekelezaji
wa mradi wa programu ya kuendeleza sekta ya Kilimo na uvuvi (AFDP).
“Nawahakikishia kuwa Ofisi ya
Waziri Mkuu ipo tayari kutoa ushirikiano wote unaohitajika ili kuhakikisha
miradi mnayoitekeleza inaleta matokeo chanya,” amesema Dkt. Kilabuko.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.