Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi amesisitiza ubunifu katika
uendelezaji wa Makao Makuu na Mji
Serikali ili kuweza kuvutia watalii wa ndani na nje.
Dkt. Yonazi ametoa msisitizo
huo wakati wa ziara yake nchini Malaysia alipotembelea Mji Mkuu wa Utawala wa
Malaysia uitwao Putrajaya.
"Ni muhimu wataalam
kuzingatia masuala yanayofanya mji wa Serikali kuwa kivutio kwa wananchi na
watalii kutoka nje. Masuala hayo ni ubunifu katika majengo, utunzaji wa
mazingira na miundombinu na huduma muhimu hasa nyumba za ibada, huduma za fedha
na maeneo ya kupumzika" amesema Dkt. Yonazi.
Aidha, Dkt. Yonazi ameahidi kuendelea kuimarisha
ushirikiano na taasisi za Kimataifa ili kubadilishana uzoefu na kujifuza masuala
ambayo yataongeza tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya
Waziri Mkuu na Serikali kwa ujumla.
Katika ziara hiyo Dkt. Yonazi
ameambata na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Mhe. Dkt. Mahadhi Maalim,
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali Bw. Paul
Sangawe, Wataalam kutoka Ubalozi wa Tanzania Nchini Malaysia na kutoka Ofisi ya
Waziri Mkuu.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.