Watumishi
wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) wameungana na
watumishi wengine wa Serikali kusherehekea Siku ya Wafanyakazi Duniani leo, Mei
1, 2026, katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Maadhimisho
hayo yameongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, ambapo
alisisitiza umuhimu wa wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na kujituma
ili kuchochea maendeleo ya taifa.
Amesema
kuwa mchango wa wafanyakazi ni msingi muhimu katika kufanikisha malengo ya
maendeleo ya nchi, hasa katika kuelekea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya
Maendeleo 2050.
Kaulimbiu
ya mwaka huu ni: “Kazi Zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika
Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050”, ikilenga kuhamasisha mazingira bora ya kazi
na ustawi wa wafanyakazi nchini.


EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.