Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge, Uratibu na wenye Ulemavu imehimiza watendaji wa Halmashauri zote za Jiji la Arusha matumizi ya Mfumo wa ukusanyaji na usimamizi wa taarifa za watu wenye ulemavu.
Hayo
yamesemwa katika Mafunzo yavitendo yaliyofanyika katika kata nne za jiji hilo
ikiwa ni muendelezo na hitimisho la mafunzo ya mfumo wa PD-MIS
yaliyowakutanisha wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na maafisa ustawi wa
jamii na TEHAMA jutoka Halmshauri zote za jiji la Arusha, yaliyochukua siku
tatu ambapo makundi ya watu mbalimbali ya watu wenye ulemavu yamejitokeza
kuitikia wito wa kujisajili katika mfumo.
Akizungumza
wakati wa kilele cha mafunzo hayo, Afisa kutoka kitengo cha huduma kwa watu
wenye ulemavu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Gerold Komba ametoa shukrani za dhati
Uongozi wa Mkoa na Maafisa ustawi wa jamii na Maafisa TEHAMA kwa kushiriki
kikamilifu katika mafunzo hayo tangu siku ya kwanza, Aidha aliwapongeza baadhi
ya watu wenye ulemavu waliojitokeza kushiriki .
Amesisitiza
kuwa ujuzi uliopatikana utakuwa nguzo muhimu katika kutekeleza majukumu ya
msingi ya ukusanyaji wa na usimamizi wa taarifa za watu wenye ulemavu.
Mafunzo
haya yanatazamwa kama hatua ya kimkakati ya kuhakikisha Maafisa na
Watendaji wanakuwa na uelewa mpana wa
kutekeleza majukumu yao katika kuwahudumia watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja
na kukusanya na kusimamia taarifa za watu wenye ulemavu mkoani humo,jambo
litakalosaidia kuimarisha upatikanaji wa
takwimu sahihi na kuimarisha na kuobresha upatikanji wa huduma kwa watu wenye
ulemavu na kuinua Uchumi kwa watu wa Kundi hili.


EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.