Watumishi
wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) wamejengewa
uwezo katika usimamizi wa mawasiliano kwa wananchi na mbinu bora za kuhudumia
wananchi pamoja na matumizi ya mifumo ya kisasa ya National call centre.
Mafunzo
hayo yamefanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Muwezeshaji Bw. Willynevilline
Msamo kutoka Benki ya NMB alieleza umuhimu uwezo wa kushughulikia mawasiliano
kwa ufanisi na kuongeza kasi ya utoaji wa huduma ili kuhakikisha kila mwananchi
anayewasiliana na taasisi anapata msaada unaostahili kwa wakati.
“Uanzishwaji
na uimarishaji wa huduma za call centre, Ofisi ya Waziri Mkuu unalenga kutatua
changamoto za wananchi kwa haraka kwa kuweka mfumo rahisi na wa moja kwa moja
wa kupokea na kushughulikia maoni, malalamiko na mapendekezo yao,” alifafanua
Aidha huduma
hii itawawezesha wananchi kupata mrejesho kwa wakati, kufuatilia masuala yao
kwa ufanisi, pamoja na kuongeza uwazi na uwajibikaji katika utoaji wa huduma za
serikali.
Bw,
Msamo alisema, “hatua hii inaonesha dhamira ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya
kuendelea kuboresha mifumo ya mawasiliano na kuhakikisha huduma zinawafikia
wananchi kwa haraka, kwa ufanisi na kwa viwango vya juu zaidi”.

EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.