Serikali
imezindua Kikosi Kazi cha Taifa cha Ufuatiliaji, Tathmini na Utoaji Taarifa
(ME&R National Task Force) kwa lengo kuratibu utekelezaji wa Mwongozo
Jumuishi wa Ufuatiliaji na Tathmini katika kusimamia utendaji wa shughuli za
Serikali.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. James Kilabuko
wakati akifungua Kikao Kazi Cha Kikosi Kazi cha Taifa cha Ufuatiliaji,
Tathmini na Utoaji Taarifa (ME&R National Task Force) kilichofanyika mkoani
Morogoro.
Dkt.
Kilabuko amesema, Ufuatiliaji na Tathmini ni dhana muhimu ya usimamizi
inayotumika kwa lengo la kuhakikisha uwajibikaji na uwazi katika utekelezaji wa
afua za maendeleo.
“Kikosi
Kazi hiki kitakuwa chombo cha kitaalamu cha kusaidia kuratibu utekelezaji wa
Mwongozo Jumuishi wa U&Tc, kuoanisha mifumo ya kitaifa ya utendaji,
kuimarisha ubora wa takwimu na taarifa za Serikali na kuandaa mapendekezo ya sera na maboresho ya
kiutendaji” alisema Naibu Katibu Mkuu huyo.
Ameeleza
kuwa, kikao kazi hicho ni fursa ya kipekee ya kujifunza, kubadilishana uzoefu
na kuweka mikakati ya pamoja ya namna bora ya kutekeleza majukumu ya Ufuatiliaji na Tathmini nchini.
“Matarajio
yangu ni kwamba, baada ya kikao hiki tutaboresha uratibu na kuoanisha viwango
vya kitaifa vya Ufuatiliaji na Tathmini (M&E) katika Wizara, Idara na
Wakala (MDAs), Sekretarieti za Mikoa (RSs) na Mamlaka za Serikali za Mitaa
(LGAs) ni hatua muhimu katika kuhakikisha uwiano na ufanisi wa utekelezaji wa
shughuli za maendeleo” amefafanua.
Vilevile, Dkt.
Kilabuko amebainisha kuwa ipo haja ya
kuoanisha viashiria vya taasisi na maeneo muhimu ya matokeo ya Kitaifa
ili kuhakikisha kuwa juhudi za taasisi mbalimbali zinaendana na vipaumbele vya
Taifa.
“
Katika hili, ni muhimu kuimarisha mwingiliano na utangamano wa Mfumo wa Kupima
Utendaji Kazi wa Watumishi wa Umma na Taasisi (PEPMIS), PIPMIS na Mfumo wa
Kitaifa wa Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo na Programu (NPMIS) ili kuwezesha
mtiririko mzuri wa taarifa na matumizi ya data kwa ufanisi” ameeleza.
.jpeg)

EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.